Monday, March 5, 2018

Zari Amuamshia Dude Upya Hamisa Mobetto


Baada ya kuchuniana kwa muda, vita ya maneno kati ya Zari The Boss Lady na Hamisa Mobetto inaonekana kuibuka upya.

Safari hii Zari ametumia mtandao wa Snapchart kutupa madogo kwa Hamisa akielezwa kuchangazwa kwake na Hamisa kujiona mdogo na mrembo lakini hawezi kuwa na mwanaume (mpenzi) wa kwake pekee yake na hata akiwa naye hawekwi hadharani.

Pia katika post hizo za Zari anaoneka kuitangaza TV Show yake ambayo ipo mbioni. Hivi karibuni katika mahojiano na Idhaa ya Kiswahili ya BBC, Zari alisema show yake hiyo itatambulika kwa jina la Life Of Zari The Boss Lady.

Pia katika posti nyingine Zari anaoneka kujibu kauli ya Hamisa ambayo alidai alikuwa katika mahusiano kwa kipindi cha miaka tisa na Diamond, Zari amechukulia jambo hilo kama ni upumbavu wa Hamisa.Beef kati ya Zari na Hamisa lilianza pale ilipogundulika kuwa Hamisa amezaa na Diamond wakati akijua muimbaji huyo yupo katika mahusiano na Zari na tayari walikuwa wameshajaliwa watoto wawili, Tiffah na Nillan.


Share:
Weka Maoni yako Hapa

0 facebook:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © MCHAMBUZI HURU | Powered by Blogger