Saturday, March 10, 2018

Wema Sepetu Si Mtu Wa Mchezo Amfanyia Unyama Mama Kanumba


Hii siyo sawa! Ndivyo unavyoweza kusema kufuatia mrembo wa sinema za Kibongo, Wema Sepetu hivi karibuni kudaiwa kumfanyia kitu mbaya mama wa marehemu Steven Kanumba, Flora Mtegoa kwa kumuita nyumbani kwake Salasala jijini Dar kisha ‘kumchomesha mahindi’ getini.

TUJIUNGE NA MAJIRANI

Ijumaa lilizungumza na mmoja wa majirani wa Wema walioshuhudia tukio hilo ambao walimuonea huruma mama Kanumba kwani, mbali ya kuwa mtu mzima, Wema aliwahi kuwa mchumba wa marehemu Kanumba hivyo haikuwa busara ‘kumchomesha mahindi getini’ kwake. “Nimeumia kweli. Mama wa watu alituambia kuwa aliwasiliana na Wema, akamuambia aje nyumbani wazungumze sasa amefi ka hapa, geti halifunguliwi,” alinukuliwa Abdul Ndeki, mmoja wa majirani.

MWINGINE ANENAJirani mwingine aliyejitambulisha kwa jina moja la Msodoki, alisema siku hiyo walishtushwa sana na kitendo cha Wema kutofungua geti kwa mtu kama mama Kanumba. “Sisi majirani hapa tumeshamzoea, hata ugonge vipi geti hawezi kukufungulia kama huna ‘apointment’ naye. “Sasa kwa mama Kanumba ndio imetushangaza sana. Huyu mama tunafahamu alikuwa mkwewe, kuja kwake hapa tunaamini kwamba pamoja na kuzungumza naye, pengine angepaswa hata kumsadia chochote kitu sasa kweli amefi ka tangu mchana hadi jioni Wema hafungui geti, hii ni sawa na kujitafutia laana,” alisema jirani huyo.HUYU HAPA MAMA KANUMBA

Akizungumza na gazeti hili kwa uchungu mama huyo alisema kuwa, aliongea na Wema hivi karibuni kwa njia ya simu na wakakubaliana aende nyumbani ambapo kesho yake alikodi Bajaj mpaka nyumbani hapo lakini alipofi ka kila alipokuwa akimpigia simu akawa hapokei hata alipojaribu kugonga mlango, walinzi walimuambia hawajapewa maagizo yoyote. “Jamani inauma mtu nimekubaliana naye vizuri, unakodi Bajaj mpaka kwake kulivyo mbali lakini hajali wala hapokei simu na nikaamua kuondoka zangu,” alisema mama Kanumba.


Marehemu Steven Kanumba.

AZIDI KUTIRIRIKA

Akizidi kuzungumza kwa uchungu, mama Kanumba alisema baada ya kukaa nyumbani hapo kwa muda mrefu bila mafanikio, alilazimika kuondoka na hata hivyo, Wema hakuona hata sababu ya kumuomba radhi kwa kilichotokea. “Yani hakuona hata umuhimu wa kuomba msamaha kwamba hakuweza kuonana na mimi labda kwa sababu fulani lakini wapi. “Mimi nilikuwa nampenda sana Wema na sijawahi kumfanyia chochote kibaya lakini kwa kitendo kile kiliniuma sana,” alisema mama Kanumba.MAZUNGUMZO YAO YALIHUSU NINI?

Alipoulizwa kuhusu alichokuwa anataka kuzugumza na Wema, mama Kanumba alisema: “Yani ilikuwa ni mazungumzo ya kawaida tu. Ni mtu ambaye kama mtakuwa mnafuatilia, kila nilipokuwa nahojiwa katika vyombo vya habari, nilikuwa namuongelea Wema kwa mazuri kama mkwe mwema, sababu nampenda lakini kwa hili alilonifanyia, sina la kusema kwa kweli lakini nimeumia sana, tena sana,” aliongea kwa masikitiko mama Kanumba.WEMA ANASEMAJE?Kufuatia madai hayo mazito ya mama Kanumba, mwandishi wetu alimtafuta Wema kupitia simu yake lakini iliita bila kupokelewa. Hata mwandishi huyo alipojaribu kwenda nyumbani kwake, aliishia getini baada ya kugonga kwa muda mrefu bila kufunguliwa. Jitihada za kumtafuta Wema zinaendelea ili afungukie madai hayo ya kumfanyia mama Kanumba kitu mbaya.MTASHA AMFUTA MACHOZI MAMA KANUMBAMara baada ya kutendewa kitu mbaya, siku chache baadaye, mtasha aliyejulikana kwa jina la Mona Zeuz ambaye anaishi nchini Dubai, alifi ka nchini na kumfuta machozi mama Kanumba. ALIANZIA MAKABURINI Mtasha huyo ambaye alijitambulisha kuwa alikuwa mtu wa karibu na marehemu Kanumba, alianzia kuzuru kaburi la Kanumba ambapo aliangua kilio kwenye kaburi hilo lililopo maeneo ya Kinondoni jijini Dar es Salaam. MREMBO HUYO NI NANI? Akijitambulisha kwa Ijumaa, mrembo huyo alisema ana asili ya Tanzania na Ujerumani, akaweka wazi kwamba, tangu kitambo alikuwa ameweka ahadi ya kuja kuliona kaburi la Kanumba kwani huko nyuma walikuwa ni marafi ki sana.AONGOZANA NA NDUGU ZAKEKatika ziara yake makaburini, msichana huyo wa kitasha aliongozana na ndugu zake watatu ambapo baada ya kufi ka tu alianza kupiga magoti huku machozi yakimtoka na wakati wote alionekana akilishika kaburi hilo na kulipapasa.AWEKA SHADA LA MAUAMrembo huyo baada ya kulia kwa muda alichukua shada lake la maua na kuliweka kaburini hapo ambapo alipomaliza zoezi hilo ndipo alipofunga safari hadi Kimara-Temboni, nyumbani kwa mama Kanumba ambapo napo alipoingia ndani tu alianza kuangusha kilio kwa uchungu huku mama huyo naye kujikuta akilia.MAMA KANUMBA AMSHUKURU

Baada ya kulia kwa muda na mtasha huyo kueleza kwa kina ukaribu wake na marehemu Kanumba (urafi ki wa kawaida), mama Kanumba alimshukuru kwa kufi ka kumuona na kusema anaumizwa na wageni wanaokuja kutoka mbali kwa ajili ya mwanaye kuliko wazawa.


AMFANYIA KUFURU

Baada ya mazungumzo mafupi na mama Kanumba kueleza changamoto mbalimbali anazopitia na kumgusia alichofanyiwa na Wema hivi karibuni, Mona aliamua kumpa ofa ya kwenda naye nchini Oman, kwa ajili ya kupumzika kidogo kuondoa mawazo au hata kuonana na sura za watu wengine wapya angalau ajisikie vizuri. Mona alisema kuwa amekuwa na ndoto ya muda mrefu ya kuja kuona kaburi la Kanumba, anamshukuru sana Mungu kwa kuweza kulitimiza hilo.“Nilitingwa sana na masomo lakini kimsingi nilikuwa nikiumia sana kutokana na msiba wake ndio maana niliweka nadhiri ya wazi kabisa nitakapomaliza masomo yangu lazima nifanye ziara hiyo na nifi ke mpaka kwa mama, Kanumba tulijuana kwenye mtandao wa kijamii wa Facebook lakini tulishibana sana,” alisema Mona.
Share:
Weka Maoni yako Hapa

0 facebook:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © MCHAMBUZI HURU | Powered by Blogger