Saturday, March 17, 2018

Wema Sepetu Ashindwa Kuficha Hisia Zake Amuandikia Ujumbe Mzito Diamond


STAA wa sinema za Kibongo, Wema Sepetu amevunja ukimya na kuamua kumwandikia ujumbe mzito huku akimwagia misifa mpenzi wake wa zamani na msanii wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platinumz’.

Wema amefunguka hayo, kufuatia Diamond kuachia ngoma mpya aliyomshirikisha msanii wa Marekani, Omario inayoitwa AFRICAN BEAUTY huku akimsifia namna wimbo huo ulivyo bora na jinsi alivyommezesha maneno ya Kiswalihi staa huyo wa Marekani.

Baadhi ya mashabiki wamedai huenda Queen huyo wa Bongo Movies anatengeneza mazingira ya kurudi rasmi kwa mpenzi wake huyo ambaye hivi karibuni ameachana na mama watoto wake, Zari The Bossy Lady kwa kile kilichodaiwa sababu kuwa Diamond amezaa na mwanamitindo Hamisa Mobeto.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Wema ameandika ujumbe huu kwa Diamond;

All dat Said… Let’s get back to Reality…. Chibu, Unaweza…!!!Chibu, Unajua….!!! Keep Doin wat you do and Live Your Dream… Bonge moja la Track… Na Hongera kwa kummezesha Omarion Swahili… I can imagine kazi uliokuwa nayo… 😅… Salute kwako… . . . The Video be on Youtube Ladies & Gentlemen… I keep Repeating it wallahy… link on his Bio @diamondplatnumz @diamondplatnumz @diamondplatnumz @diamondplatnumz … . . . Picha twazitwanga Kisela, Post insta wanga kuwakera….😅😅😅 Tatizo wanga wa Insta hawakawii kukukera wewe… 😅😅😅 . . . #AFRICANBEAUTY 😝
Share:
Weka Maoni yako Hapa

0 facebook:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © MCHAMBUZI HURU | Powered by Blogger