Saturday, March 17, 2018

Waziri Mwakyembe Amlilia Mpiga Picha wa ITV


Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe kilichotokea Machi 16, mwaka huu katika Hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar Es Salaam.

Waziri Mwakyembe kupitia taarifa yake aliyoitoa kwa vyombo vya habari ameeleza kupokea kwa masikitiko kifo cha mpiga picha huyo Mkongwe wa ITV.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe amepokea kwa masikitiko taarifa ya kifo cha Mpiga Picha mkongwe Bw. Evarist Ottaro kilichotokea jana tarehe 16 Machi, 2018 katika Hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar Es Salaam.

Dkt. Mwakyembe ameeleza kuwa kifo cha Bw. Ottaro kimeipokonya tasnia ya Habari mmoja wa Wapiga Picha mahiri waliokuwa tegemeo kubwa la maendeleo ya tasnia hiyo nchini.

Dkt. Mwakyembe ametoa pole kwa familia, uongozi wa Kituo cha Televisheni cha ITV, ndugu, jamaa, marafiki na wanahabari wote nchini na kuwaombea Mungu awape faraja katika kipindi hiki kigumu cha msiba.

Wakati wa uhai wake Bw. Ottaro amewahi kufanya kazi na vituo vya Televisheni vya Channel Ten na DTV kabla ya kuhamia katika kituo cha Televisheni cha ITV ambapo amefanya kazi kwa miaka kumi na saba hadi alipofikwa na umauti.

Imetolewa na:

Lorietha Laurence
Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo.
17/03/2018.
Share:
Weka Maoni yako Hapa

0 facebook:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © MCHAMBUZI HURU | Powered by Blogger