Sunday, March 4, 2018

Waziri Atolea Ufafanuzi Kichwa cha Treni Ambacho kilipata Ajali


Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof.Makame Mbarawa amefunguka na kutolea maelezo juu ya kichwa cha treni ambacho kilipata ajali Februari 28, 2018 na kuhusishwa na moja ya vichwa vya treni ambavyo vilikutwa havina mwenyewe na Rais Magufuli. 

"Kichwa kilichopata ajali ni moja ya vichwa ambavyo vilikuja mwaka mmoja uliopita hakikuwa bandarini na hivi vilivyopo sasa hivi, vilivyopo sasa vina namba kuanzia 9014 mpaka 9024 tuwe angalau tunatumia weledi kwenye kazi zetu. Picha iliyounganisha si miongoni mwa vichwa vya sasa vilivyopo bandarini nina imani teknolojia inaweza saidia maana yenyewe inatunza hebu google tu hiyo picha uangalie ni ya mwaka gani ili Kupata jawabu sahihi" alisema Mbarawa 


Miezi kadhaa iliyopita Waziri huyo aliweka wazi nia ya Serikali kutaka kuvinunua vichwa hivyo vya treni 11 ambavyo vilikuwa vikisemekana kuwa havina mwenyewe na kudai kuwa walianza mazungumzo na muhusika ili kuona wanawezaje kufanya biashara. 
Share:
Weka Maoni yako Hapa

0 facebook:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © MCHAMBUZI HURU | Powered by Blogger