Friday, March 2, 2018

Watuhumiwa Mauwaji ya Kiongozi CHADEMA Wadakwa


Watu 13 wanashikiliwa na Polisi mkoani Morogoro kwa makosa mawili tofauti wakiwemo 11 kwa tuhuma za kuhusika katika tukio la kifo cha Diwani wa CHADEMA huku wengine wawili raia wa Kenya wakishikiliwa kwa tuhuma za utapeli wakijifanya wao ni (TRA).

Kwa mujibu wa kamanda wa Polisi mkoa wa Morogoro, Ulrich Matei amesema baada ya tukio la kuuwawa kwa Diwani wa Kata ya Namwawala wilaya ya Kilombero Godfrey Luena, Jeshi la Polisi mkoani humo liliendesha msako wa kuwabaini wahusika wa tukio hilo ambapo mpaka sasa jumla ya watu 11 wanashikiliwa kwa tuhuma za kuhusika na mauaji hayo.

Katika hatua nyingine, watu nwawili ambao ni raia wa Kenya wanashikiriwa na polisi Mkoani humo kwa tuhuma za kujihusisha na utapeli kwa kujifanya ni mawakala wa mamalaka ya mapato nchini.

Share:
Weka Maoni yako Hapa

0 facebook:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © MCHAMBUZI HURU | Powered by Blogger