Tuesday, March 6, 2018

Watu 9 Washikiliwa na Jeshi la Polisi kwa Kudhaniwa kuwa ni Wahamiaji Haramu


Watu tisa wanaodhaniwa kuwa ni wahamiaji haramu wamekamatwa na Jeshi la Polisi Mkoani Mwanza kwa tuhuma za kuingia nchini Kinyume cha sheria.

Watuhumiwa hao wamekamatwa katika eneo na Nyashishi Wilayani Msingwi Mkoani humo wakiwa wamejificha katika vichaka kwa ajili ya kwenda kuchukuliwa kwa ajili ya kuendelea na safari yao.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mwanza, Ahmed Msangi amesema kuwa kukamatwa kwa raia hao kunafuatia taarifa za raia mwema aliewatilia shaka na kisha kutoa taarifa kwa jeshi la polisi juu ya watu hao waliojificha katika kichaka hicho.

Katika hatua nyingine Kamanda Ahmed Msangi amewataka wananchi kutanguliza uzalendo kwa kuwafichua watu wanaoshi nchini bila ya kuwa na vibali maalumu na kinyume cha sheria.
Share:
Weka Maoni yako Hapa

0 facebook:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © MCHAMBUZI HURU | Powered by Blogger