Thursday, March 15, 2018

WASTARA Sajuki Ajutia ndoa yake na Mbunge wa CCM


Muigizaji na Mfanyabiashara, Wastara Juma amesema kwenye maisha yake mwanaume anayejutia kuwa naye kwenye mahusiano ni Mbunge wa jimbo la Donge, Sadifa Khamis Juma kwani hakumjua vizuri kabla ya kukubali kufunga naye ndoa.


Akizungumza leo kwenye  kipindi cha KIKAANGONI kinachorushwa kupitia ukurasa wa facebook wa EATV kila siku ya Jumatano kuanzia saa nane mchana mpaka saa kumi jioni, ambapo amesema kwamba alikubali kufunga ndoa na mwanaume huyo pasipo kumjua ni mtu wa aina gani.

"Najuta kuwa na mahusiano na Sadifa kwa sababu sikuwa namjua vizuri. Tulifunga ndoa baada ya kujuana kwa kipindi cha wiki moja. Alikuja kwa njia ya kunipa faraja kwa vile mimi ni yatima, pia mjane lakini pia ni mlemavu. Mtu mimi akiniambia kitu kama hicho anaweza kuiteka akili yangu kabisa," Wastara.

Hata hivyo Muogizaji huyo amesema kuwa moja ya sababu kubwa kuachana na mumewe Sadifa ilikuwa ni pamoja na mumewe huyo kulazimisha apewe risiti zote alizokwenda nazo kwenye matibabu kwa fedha alizochangiwa na Alikiba, Makamu wa Rais Mama Samia ili yeye akalipwe fedha zote na Bunge.
Share:
Weka Maoni yako Hapa

0 facebook:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © MCHAMBUZI HURU | Powered by Blogger