Friday, March 9, 2018

Wanawake ndio Waathirika Wakubwa wa Mabadiliko ya Tabia ya Nchi


Tanzania kama nchi nyingine duniani zinakabiliwa na tatizo la mabadiliko ya Tabia ya Nchi na kutokana na tatizo hilo, Mkurugenzi wa Kituo cha Sayansi ya Tembo Dk. Alfred Kikoti mwezi July, 2017 alitoa tahadhari kuwa kutokana na mabadiliko hayo kuna hatari ya nchi kubakiwa na hifadhi 2 kati ya 16 ifikapo mwaka 2050.

Hata hivyo taarifa iliyotolewa na Umoja wa Mataifa siku za hivi karibuni ni kwamba wanawake ndio waathirika wakuu wa mabadiliko haya ya tabia ya nchi kuliko wanaume.

Takwimu za Umoja wa Mataifa zinaonesha kuwa asilimia 80 ya watu ambao wanalazimika kuhama kutoka eneo moja kwenda eneo jingine kutokana na mabadiliko ya tabia ya nchi ni wanawake.
Share:
Weka Maoni yako Hapa

0 facebook:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © MCHAMBUZI HURU | Powered by Blogger