Monday, March 5, 2018

Wananchi Wapiga Kura Uchaguzi Mkuu Italia


Watu nchini Italia wanapiga kura baada ya kampeni zilizoangazia zaidi masuala la uhamiaji na uchumi.

Waandishi wa habari wanasema kuwa ni vigumu kusema ni nani atashinda katika kura hiyo.

Upande wa Five Star Movement, chama kinachotawaka, na mrengo wa kulia wa waziri mkuu wa zamani Silvio Berlusconi wote wametabiri ushindi.

Bw Berlusconi, 81, hawezi mweyewe kushika wadhifa wowote hadi mwaka ujao kutokana na kesi inayohusu kodi.

Kura za maoni zilipigwa marufuku wiki mbili zilizopita lakini uatafiti kabla ulionyesha kuwa muungano huo wa Berlusconi ulikuwa na nafasi ya kupata ushindi.

Uhamiaji

Zaidi ya wahamiaji 600,000 wamefanya safari kutoka Libya wakipitia bahari ya Mediterranean na kuwasilia Italia tangu mwaka 2013.

Idadi hiyo kubwa imewakasirisha watu wengi nchini Italia.

Bw Berlusconi amataja wamamiaji hao kuwa bomu linalosubiri kulipuka na kuahidi kuwa atawakufukuza wengi.

Uchumi

Uchumi wa Italia umeanza kupanuka kwa mara nyingine lakini miaka 10 ya kuwepo hali mbaya ya uchumi wa dunia, pato la taiafa linasalia asilimia 5.7 chini kabla ya hali hiyo.

Mwaka 2016 takriban watu miloni 18 walikuwa kwenye hatari ya kukumbwa na umaskini na ukosefu wa ajira ulikuwa asimia 11.

Share:
Weka Maoni yako Hapa

0 facebook:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © MCHAMBUZI HURU | Powered by Blogger