Tuesday, March 6, 2018

Wanachama wa Shirika la Diaspora Afrika Kusini Waandamana Kubaini Ukweli wa Kifo cha Mwanafunzi Mtanzaninia Aliyeuawa


Leo March 6, 2018 Wanachama wa Shirika la Africa Diaspora Forum wamefanya maandamano nchini Afrika Kusini kushinikiza serikali ya nchi hiyo na ya Tanzania kubaini ukweli kuhusu kuuawa kwa mwanafunzi raia wa Tanzania mwezi February.

Baraka Leonard Naferi, mwanafunzi wa shahada ya uzamifu, alifariki baada ya kugongwa na gari la nje ya bweni la chuo kikuu.

Maafisa wa shirika hilo wameandamana kwa pamoja na baadhi ya wanafunzi na wafanyakazi wa Chuo Kikuu cha Johannesburg nje ya bweni linaloitwa Sophiatown ambapo mwanafunzi huyo aligongwa na kufariki.


Maandamano hayo yalikuwa salama na watu walikusanyika kwenye uzio mahali gari lilipo mgonga marehemu Baraka Naferi wakiwa wamebeba mabango yanayosema tunataka haki kwa Baraka, haki itendeke kwa Baraka.

Mtuhumiwa alikamatwa na polisi wa Afrika Kusini lakini baadaye akaachiliwa huru kwa dhamana. Polisi walisema hakukuwa na ushahidi wa kutosha wa kumfungulia mashtaka ya mauaji.
Share:
Weka Maoni yako Hapa

0 facebook:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © MCHAMBUZI HURU | Powered by Blogger