Friday, March 9, 2018

Wachina Wapagawa na Wowowo la 'Aunty Lulu'


KATIKA hali ya kustajabisha, Wachina ambao hawakuweza kufahamika majina yao, wamenaswa wakipagawa na kugombea kumshika kalio, mtangazaji maarufu Bongo, Lulu Semagongo ‘Aunty Lulu’ nchini China.

 Mrembo huyo amekwenda nchini humo hivi karibuni ambapo tukio hilo lilitokea alipohudhuria shoo ya mwanamuziki wa Tanzania anayeishi nchini humo aitwaye Zitha, iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Shenzhen.
Kwenye video nilyoipata, ilimuonesha Aunty Lulu akigombewa na Wachina hao huku wengine wakionekana kumrekodi video kupitia simu zao ambapo wengi walionekana kuvutiwa zaidi na kalio kubwa la Aunty Lulu.

“Unajua wameshangazwa na kalio langu huku wanawake wao hawana makalio hivi, niliona wanacheza nikainuka kucheza nao hilo lilikuwa ni kosa kwangu walipagawa ile mbaya,” alisema Aunty Lulu.
Wachina hao walikuwa wakimgombea huku wengine wakiomba kupiga naye picha na wakati walipokuwa wakipiga naye picha, kila mmoja alikuwa akimgusa kalio.
Share:
Weka Maoni yako Hapa

0 facebook:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © MCHAMBUZI HURU | Powered by Blogger