Monday, March 5, 2018

Wabotswana Watamba Kuijua Yanga


Kocha wa timu ya Township Rollers ya Botswana ambayo ipo nchini kwaajili ya mchezo wa ligi ya Mabingwa Afrika, kesho dhidi ya Yanga Nikola Kavazovic, amesema anafuatilia soka la Afrika ikiwemo klabu ya Yanga.

"Nimekuwa nikifuatilia soka la Afrika, kabla ya mchezo wetu na Yanga tumeangalia michezo yao minne miwili ya nyumbani na miwili ya ugenini hivyo tunafahamu tutacheza na mpinzani wa aina gani" amesema kocha huyo raia wa Serbia.

Kavazovic ameongeza kuwa mbali na Yanga lakini pia anafuatilia soka la Tanzania na anafahamu klabu mbalimbali zikiwemo Simba SC na Azam FC ambazo amezitaja kuwa ni miongoni mwa timu bora katika bara la Afrika.

Naye nahodha wa Township Rollers Maano Ditshupo akiongelea mchezo wa kesho kwenye mkutano na wanahabari makao makuu ya TFF amesema wao kama timu wapo tayari kwa mchezo huo na wamejiandaa kupata matokeo mazuri.

Mchezo huo wa kwanza utachezwa kesho saa 10 jioni kwenye uwanja wa taifa jijini Dar es salaam kbala ya timu hizo kurejeana wiki moja baadae ambapo Yanga itasafiri kwenda nchini Botswana.

Share:
Weka Maoni yako Hapa

0 facebook:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © MCHAMBUZI HURU | Powered by Blogger