Friday, March 9, 2018

Uvumilivu Wamshinda Witness Kibonge Ataja Wanaume Wanaomvutia


Msanii wa muziki wa Bongo Fleva, Witness ameamua kuweka wazi hisia zake kwa kuuelezea umma kuwa hata yeye anavutiwa na watu maarufu ila kwa utofauti na wanawake wengine.

Witness amesema kuwa mara nyingi anapenda kutembelea kwenye kurasa za mitandao ya kijamii ya watu maarufu anaowapenda zaidi duniani na kutazama maisha yao huku akiwaombea wafanikiwe kwenye kazi zao.

Akielezea upendo huo, Witness amesema yeye yupo tofauti na wanawake wengine ambao wakiwaona watu maarufu wanatamani kutoka nao kimapenzi, bali upendo wake ni kuona watu maarufu wanaomvutia wakiwa na furaha na kufanikiwa zaidi.

“Huwa ninajishangaaje mimi ni binadamu wa aina gani? Wanawake wengi wakiwapenda mastaa, haijalishi ni wa movie, muziki mpira ama kitu chochote kile, hutaka kuduu nao, But mimi nikimpenda staa au mtu sana anayefahamika huwa ninapenda kumuona, akifanikiwa zaidi pia hupenda awe na maisha mazuri na mwanamke mzuri ampendae yeye hata nikipita kwenye kurasa zao ninaona wana happy faces as a family I get to love them all and respect there women for loving the stars I love! Coz huwachukulia kama my blood brothers,“ameandika Witness kwenye ukurasa wake wa Twitter na kutaja orodha ya wanaume anaowapenda zaidi.

“ Mtu wa Kwanza ninayempenda bure na kumfurahia ni 1.@cristiano (Cristiano Ronaldo-Ureno) 2.@bustaryhmes (Busta Rhymes-Marekani) 3. @simplyluca (Luca Neghest-Tanzania) “ameandika Witness.

Hata hivyo ni hisia tu ya kawaida ambayo kila binadamu anakuwa nayo kwani kwenye orodha hiyo ya watu aliowataja, wote wana wenza wao na wanaishi na familia zao.
Share:
Weka Maoni yako Hapa

0 facebook:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © MCHAMBUZI HURU | Powered by Blogger