Monday, March 12, 2018

Unaambiwa Michael Ballack Alikuwa Ananuka Hadi Akawa Anakimbiwa Uwanjani


“Dunia ina mambo” ndivyo unavyoweza kuanza kusema kutokana na madai yaliyotolewa na golikipa wa zamani wa timu ya taifa ya Paraguay kuhusu kiungo wa zamani wa Chelsea na timu ya taifa ya Ujerumani Michael Ballack.

Sijui ni chuki kutokana na kuondolewa na Wajerumani katika kombe la dunia 2002 au ni kweli lakini Jose Luiz Chilavert amedai ya kwamba kati ya sababu kubwa wachezaji walikuwa wakimhofia Ballack ilikuwa harufu.

Chilavert amesema ni kweli Ballack alikuwa na nguvu sana uwanjani lakini hilo silo kubwa lililokuwa likifanga wachezaji wengine wamhofie, lakini ukweli ni kwamba Michael Ballack alikuwa akitoa harufu kali sana mwilini.

Akiongea na kituo cha ESPN Chilavert aka Bulldog amesema kwamba ulikuwa ukimkaribia Ballack unasikoa harufu ya malimao limao na vitu ambavyo vilikuwa na harufu kali sana hadi unakosa raha.

Hii ilikuwa ikiwakera sana haswa viungo wa Paraguay na ndio sababu Ballack alionekana bora dhidi yao kwa kuwa walikuwa hawamsogelei kabisa na Chilavert anadhani labda hii ilikuwa mbinu ya Ballack.

Chilavert ameichezea Paraguay michezo 74 kuanzia mwaka 1989 hadi mwaka 2003 lakini golikipa huyj ndio mlinda lango namba mbili mwenya mabao mengi(67)lakini ndio mlinzi pekee ambaye amewahi kufunga hattrick, ilikuwa 1999 wakati akiichezea Vélez Sarsfield.

Share:
Weka Maoni yako Hapa

0 facebook:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © MCHAMBUZI HURU | Powered by Blogger