Friday, March 9, 2018

Siri Nzito na ya Kutisha Nyuma ya Mataifa Makubwa Yanayomiliki Wanasayansi Bora Wa Anga Duniani.


KWA miaka takriban 100 sasa dunia imeshindwa kutengua kile kinachoonekana kuwa kitendawili kigumu, kuhusu kuwepo Vyombo vya Anga maarufu kwa jina la UFO.
UFO ni 'Unidentified Flying Objects,' yaani Vyombo vya Anga Visivyofahamika.
Mpaka wakati huu, hudaiwa na Wanasayansi wa masuala ya anga kuwa vyombo hivyo haijulikani ni wapi vinatoka kuja duniani.

Hata hivyo, yapo madai kuwa mataifa makubwa, ikiwemo Marekani, Urusi, China, Uingereza na Japan, yanafahamu chanzo cha kuwepo vyombo hivyo.
Upo uwezekano kuwa mataifa hayo yamekubaliana kutunza siri kuhusiana na UFO.
Pia zimekuwepo dalili nyingi kuonesha kuwa upo uwezekano kwa Marekani kufahamu kile kinachoendelea kuhusiana na vyombo hivyo, hususan kutokana na madai ya Wamarekani wengi kuishutumu serikali yao kuficha ukweli juu ya vyombo hivyo.
Wamarekani huishutumu serikali yao kuwa inafahamu au inahusika na kuwepo UFO, na hivyo kusababisha hofu kwao.

Miongoni mwa watu maarufu waliowahi kutaka ufanyike uchunguzi kuhusiana na UFO ni milionea Laurance Rockeffer, ambaye sasa ni marehemu.
Mwaka 1993 hadi 1995, tajiri huyo alitoa kiasi cha fedha zake kuanzisha na kuendesha kampeni ya kutaka serikali ya Rais Bill Clinton nchini Marekani iueleze umma ukweli kuhusiana na UFO.
Ingawa kimsingi serikali hiyo ilikubaliana na matakwa hayo, lakini baadaye ilielezwa kuwa uchunguzi haukubaini chanzo cha UFO.

Kadhalika, wakati wa kampeni ya kuwania Urais wa Marekani ambapo Bi Hillary Clinton alichuana na Rais wa sasa, Donald Trump, mwanamama huyo aliahidi kwendeleza uchunguzi huo dhidi ya UFO.

Hata hivyo, Clinton alibwagwa na Trump na hivyo wazo la kutafiti UFO likafa.
Miongoni mwa taasisi ambazo zimekuwa zikibanwa na umma kueleza au kuthibitisha kama UFO ni vyombo vya anga kutoka anga za mbali, ni pamoja na NASA ambalo ni shirika la anga za juu la nchi hiyo.

Kwa upande wake, shirika hilo lenye wanasayansi wa anga waliotukuka, limekuwa linakanusha kufahamu chochote kuhusiana na uwepo wa UFO.
Nchi zingine zote hazisemi chochote kuhusiana na vyombo hivyo, ingawa watu wao wamekuwa wakiviona na kuhoji serikali zao.

Kadhalika, licha ya wanaanga wa vyombo vya Apollo vilivyosafirisha binadamu 12 kwa nyakati tofauti kwenda kutua mwezini mwaka 1969 hadi 1972 kudai kuwa waliona UFO, lakini NASA hukanusha vikali.

Miongoni mwa wanaanga hao ni wale wa Apollo 11 mwaka 1969, ambao walidai kuwa wakiwa katika siku ya 3 safarini tangu kuondoka duniani (siku 1 kabla ya kuwasili mwezini), ghafla walistukia UFO inajitokeza angani na kwenda sambamba na Apollo ambayo kasi yake ilikuwa kubwa ajabu.

Kwa mujibu wa kitabu cha David Knight: "UFOs" cha mwaka 1979, mwandishi hueleza kuwa Julai 19, 1969 saa 12 jioni katikati ya anga ya dunia na mwezi, UFO ilijitokeza na kumudu kwenda na kasi ya Apollo.

Licha ya wanaanga hao kuiarifu NASA duniani kuwa chombo cha kigeni kilikuwa kimejitokeza angani na kutishia usalama wa Apollo, walijibiwa kuwa "hiyo ni UFO, achana nayo, zingatieni safari yenu, chunga muda."

Aidha, huelezwa kuwa kwa nyakati tofauti UFO zilijitokeza mara 3 dhidi ya hiyo Apollo 11, mara ya mwisho ikiwa wakati imetua mwezini; ambapo UFO ilituwa kwa mbali.
Kwa vile wanaanga wote wa Apollo zote hueleza kutokewa na UFO huko anga za juu, ngoja tugeukie eneo lingine.

Yapo machapisho ya miaka mingi yanayosimulia kuonekana kwa UFO, ambapo mwaka 1930 nchini Marekani vyombo hivyo viliripotiwa kuonekana.
Kuna kumbukumbu inayoeleza kuwa hata katika karne ya 15, UFO zilikuwepo katika anga ya dunia.
Kumbukumbu hiyo inataja Aprili 14, 1561 ambapo chombo chenye umbo la pembetatu kilionekana kuruka katika anga ya Nuremberg, Ujerumani.

Kati ya mwaka 1916 na 1926 matukio 1,305 ya kuonekana UFO yalirekodiwa nchini Marekani, mwaka 1946 matukio 2,000 katika nchini za Scandinavia, yaani Sweden, Norway, Finland, Denmark na pia nchini Uholanzi.

Hali hiyo pia imekuwa ikiripotiwa katika nchi mbali mbali, ambapo nchini Afrika ya Kusini ambayo pia huandamwa na UFO iliripoti kuonekana chombo hicho Oktoba 30, 2011.
Nao marubani wa ndege za abiria wamekuwa wakiripoti kuona UFO wakiwa safarini angani.
Katika ripoti za watafiti wa UFO duniani kote, zaonyesha kuwa mpaka wakati huu jumla ya matukio 3,500 ya kuonekana vyombo hivyo yameripotiwa na marubani wa ndege za abiria.
Aidha, mwaka 1952 ndipo jina la UFO lilipoanza kutumika nchini Marekani, badala ya jina la awali la "flying saucers" (visahani virukavyo).

Lakini pia wakati utata ukiendelea hivyo, inadaiwa na mashuhuda kuwa katika Jimbo la Nevada nchini Marekani kuna eneo la siri liitwalo No. 51 ambalo ni hifadhi ya viumbe kutoka anga za mbali na baadhi ya UFO zao.

Hudaiwa kuwa eneo hilo lenye ulinzi mkali kutoka vyombo vya ulinzi vya Marekani, lina barabara ya urefu wa kilomita 158 iitwayo "Extraterrestrial Highway" (barabara kuu ya anga za mbali), ambayo wasafiri wa kitalii huripoti kuona viumbe wenye maumbo ya kibinadamu wakiranda jirani.
Barabara hiyo ilipewa jina hilo mwaka 1996, na inadaiwa kuwa tangu mwaka 1976 shughuli katika eneo hilo zimeongezeka maradufu.

Inadhaniwa kuwa yawezekana viumbe hao ni wale ambao huripotiwa kukamatwa mateka baada ya kuanguka UFO, au pengine huenda Marekani ina "ubia" wa kiteknolojia na viumbe wa UFO kutoka anga za mbali.

Hiyo inatokana na kuwepo usiri mkubwa katika eneo hilo No. 51, ambalo hata hivyo kuwepo kwake hukanushwa na serikali ya Marekani.
Share:
Weka Maoni yako Hapa

0 facebook:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © MCHAMBUZI HURU | Powered by Blogger