Monday, March 5, 2018

Serikali Yakiri Uwepo wa Changamoto ya Usafishaji Umeme Nchini


Mkurugenzi Mkuu, Idara ya Habari – Maelezo na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbasi amekiri uwepo wa changamoto ya usafishaji wa umeme nchini baada ya kuingizwa kwenye gridi ya Taifa.

Dkt. Abbas ameyasema hayo leo, wakati akizungumza na waandishi wa habari mjini Dodoma, ambapo ameeleza kuwa kwenye umeme kuna mambo makubwa mawili ambayo ni uzalishaji na usafirishaji.

“Ndugu yangu kwenye umeme, umeme kuna mambo makubwa mawili, kuna uzalishaji na kuna usafirishaji kwa kweli tunazochangamoto za kuuzalisha umeme na ndizo ambapo nimeeleza kwa kweli kwa kiasi kikubwa tunaangalia kwa namna gani tunazitatua kwa maana ya kuazalisha umeme mwingi lakini lazima tukiri kwenye nchi yetu kuna changamoto kubwa sana ya kuusafirisha sasa, ukishauingiza kwenye gridi ya Taifa unafikaje kwako unafikaje kwenye viwanda? kwahiyo kuna changamoto kwenye mifumo kama hizi transfomer zinaungua mara kwa mara kutokana na hali mbalimbali za hewa na kipindi hiki cha mvua changamoto ndio zinaongezeka,“ amesema Dkt. Abbas wakati akijibu swali la mwandishi aliyehoji kukatika katika kwa umeme.

Ameongeza “Sasa kwa ambapo ninachoweza kukuhakikishia kwa mujibu wa uzalishaji wa umeme Tanzania na mahitaji bado tuna umeme mwingi sana kuliko mahitaji na kama tulivyoonyesha hapa miaka kadhaa ijayo tutakuwa na umeme mwingi zaidi“.
Share:
Weka Maoni yako Hapa

0 facebook:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © MCHAMBUZI HURU | Powered by Blogger