Monday, March 5, 2018

Romy Jons afunguka kufungiwa kwa nyimbo mbili za Diamond


Dj wa Diamond Platnumz, Romy Jons amefunguka kufuatia ngoma mbili za msanii huyo kufungiwa, Romy Jons akiwa official Dj wa Diamond amesema hatua hiyo inaumiza kwa namna moja au nyingine ila hawawezi kupingana na mamlaka husika.

“Lazima ujisikie vibaya lakini mwisho wa siku lazima ukubaliane na maamuzi ya serikali kwa hiyo huwezi kukataa ni sawa kwa sheria za kwao zimekataza ni kitu kizuri tunakubaliana nalo,” amesema.

Wiki iliyopita Mamlaka ya Mawasiliano Nchini (TCRA) ilitangaza kufungia baadhi ya nyimbo zilizooneka kutokuwa na maadili, miongoni mwa ngoma hizo ni Hallelujah na Waka zote za Diamond.

Share:
Weka Maoni yako Hapa

0 facebook:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © MCHAMBUZI HURU | Powered by Blogger