Thursday, March 1, 2018

Roma Mkatoliki Apigwa Kitanzi cha Miezi Sita Kisa Kibamia


Msanii wa Bongo Fleva, Roma Mkatoliki amefungiwa miezi sita kutojihusisha na Muziki ikiwa ni kutekeleza azma ya Serikali kwa kile kinachodaiwa kukiuka maadili ya jamii za kitanzania kwenye wimbo wake wa "KIBAMIA".

Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Juliana Shonza, amesema kuwa Roma amedharau wito wa serikali ambapo leo aliitwa ili ahojiwe   kutokana na wimbo wake huo ikiwa ni hatua ya pili mara baada ya Baraza la Sanaa Nchini Basata kumuita na kumtaka arekebishe baadhi ya sehemu katika wimbo huo.

"Tumempigia simu mara kadhaa hajapokea, tumemtumia meseji anasoma lakini hajibu chochote hivyo hiyo ni dharau na hatuendelei kudili na mtu mmoja wasanii ni wengi ambao wanahitaji msaada kutoka kwetu" alisema Shonza.
Share:
Weka Maoni yako Hapa

0 facebook:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © MCHAMBUZI HURU | Powered by Blogger