Friday, March 9, 2018

Ray Kigosi Amwagia Sifa Kibao Mama Mtoto wake Chuchu Hans


LEJENDARI wa sinema za Kibongo, Vincent Kigosi ‘Ray’ amemwaga sifa nyingi kwa mzazi mwenziye, Chuchu Hans, kwa kusema kuwa ni mama bora anayejua kumlea vziuri mtoto wao, Jaden.

 Akizungumza na gazeti hili, Ray alisema kuwa, Chuchu amekuwa ni mstari wa mbele katika kuhakikisha mtoto wao anakuwa na afya njema na pia anakuwa kwenye mazingira mazuri siku zote.
“Unajua angekuwa mwanamke mwingine, angeona mtoto anamzibia vitu vingi hasa kwenye upande wa kuendelea kucheza filamu, lakini aliweka pembeni lengo likawa moja tu, kumuangalia mtoto tu,” alisema Ray.

Muigizaji huyo aliongeza kuwa, anamuombea sana kwa Mungu mzazi mwenziye huyo aendelee kuwa na moyo huo wa malezi bora kwa mwanaye kwani mama ndiye hubeba kwa asilimia kubwa jukumu la malezi.

Stori: Imelda Mtema, Amani

Share:
Weka Maoni yako Hapa

0 facebook:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © MCHAMBUZI HURU | Powered by Blogger