Monday, March 5, 2018

Rais Museveni Atengua na Kuteua IGP Mpya


Rais  Yoweri Museveni wa Uganda ametengua uteuzi wa mkuu wa jeshi la polisi nchini humo IGP Generali Kale Kayihura na waziri wa usalama Generali Henry Tumukunde mara moja.

Taarifa iliyotolewa na Ikulu ya nchi hiyo leo imesema kwamba Rais Yoweri Museveni amemteuwa Okoth Ochola ambaye alikuwa Naibu Mkuu wa jeshi la Polisi  kuwa  mkuu mpya wa jeshi hilo la Polisi IGP.

Taarifa hiyo pia inasema Rais Museveni amemteuwa Geberali Elly Tumwine, kuwa Waziri mpya wa usalama akichukua nafasi iliyokuwa ikishikiliwa na Geberali Tumukunde.

Taarifa hiyo imesema Brigadia Sabiiti Muzeei ameteuliwa kuwa naibu mkuu wa jeshi la polisi nchini humo DIGP. Rais Meseveni mnamo mwezi Mei tarehe 2 alimteuwa tena Geberali Kayihura kuwa mkuu wa jeshi la Polisi kwa miaka mingine mitatu hata hivyo uteuzi huo haujatimu hata mwaka mmoja.

Share:
Weka Maoni yako Hapa

0 facebook:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © MCHAMBUZI HURU | Powered by Blogger