Friday, March 9, 2018

Rais Magufuri Ahaidi Kumpa Kazi Serikalini Dk. Kimei


Rais John Magufuli amesema licha ya kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB, Dk Charles Kimei anakaribia kustaafu ameahidi kumpatia nafasi katika Serikali ya Awamu ya Tano.

Rais Magufuli ametoa kauli hiyo leo Ijumaa Machi 9, 2018 wakati akizindua tawi la benki hiyo wilayani Chato mkoani Geita.

“Kimei wewe ustaafu tu lakini nasema nafasi bado zipo. Muda wako unamalizika CRDB lakini Serikalini bado unaweza kufanya kazi ndani ya Serikali bado upo na ninakuahidi asilimia 100,” amesema Rais Magufuli.
Share:
Weka Maoni yako Hapa

0 facebook:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © MCHAMBUZI HURU | Powered by Blogger