Tuesday, March 6, 2018

Rais Magufuli Aagiza Kuendelezwa Kwa Ujenzi wa Msikiti Uliowekewa Pingamizi


Rais John Magufuli ameagiza kuendelea kwa ujenzi wa msikiti wa ISTIQAAMA COMMUNITY katika Manispaa ya Sumbawanga Mkoani Rukwa uliokuwa umewekewa pingamizi la kujengwa kutokana na kukiukwa taratibu za ujenzi.

Akisoma agizo hilo la Rais Magufuli mbele ya viongozi wa Baraza la Waislamu Tanzania -BAKWATA, waumini na wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa, Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Jochiam Wangabo amesema uamuzi huo umezingatia kujenga amani na utulivu katika jamii.
Share:
Weka Maoni yako Hapa

0 facebook:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © MCHAMBUZI HURU | Powered by Blogger