Sunday, March 18, 2018

Q Chief Amlaumu Papii Kocha


Msanii wa BongoFleva Q Chief ameibuka na kujitetea kuwa hana tofauti yeyote ile na Papii Kocha pamoja na Nguza Vicking ila kuna baadhi ya watu ndio wanataka kuwatia ubaya kuhusiana na kuzimiwa MIC akiwa kwenye jukwaa akitumbuiza.


Q chief ametoa kauli hiyo akiwa anazungumza kwenye kipindi cha eNewz inayorushwa na tinga namba moja kwa vijana EATV baada ya kupita siku kadhaa tokea msanii huyo kuzimiwa MIC kwenye 'show' ya kuwakaribisha kwa mara nyingine katika tasnia ya muziki Papii na mzee Nguza kutokana na kupotea kwa miaka mingi kwa machoni mwa mashabiki na wapenda burudani wa dansi.

"Wakati mimi nina 'perfom' wimbo wangu wa kwanza katika 'show' wa nikilala naota, nilipata baraka zote kutoka kwa MC wa shughuli, Papii na Baba pia. So kwenye kazi unapoona watu wanamuitikio mzuri inabidi ujiongeze kutokana na wao kuonesha mapenzi yao hivyo mimi nimefanya kazi yangu kama vile ninavyofanya sehemu nyingine kwasababu nina nguvu nyingi katika kazi zangu lakini baadae wakati napanda juu nikashangaa kati kati ya wimbo nimezimiwa kipasa sauti 'MIC'", amesema Q chief.

Pamoja na hayo, Q chief ameendelea kwa kusema "sitaki kuweka kama kulikuwa na tofauti lakini kama zilikuwepo basi nilikuja kujizua baada ya kuangalia zile video tena na watu wa karibu pamoja na mke wangu kuniuliza ni jambo gani lilikuwa linaendelea mpaka kutokea vile. Lengo langu lilikuwa ni kutoa burudani, kumfariji rafiki ambae alipotea machoni mwangu kwa muda mrefu kwa mapenzi yote lakini MIC ikazimwa, sio kosa la Papii wala Mzee wangu Nguza kwasababu wao hawaitahi 'stress' bali ni kosa la ambaye alikuwa fundi mitambo 'technical' aliyekuwepo nyuma anashughulikia masuala ya vyombo vyote"
Share:
Weka Maoni yako Hapa

0 facebook:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © MCHAMBUZI HURU | Powered by Blogger