Friday, March 16, 2018

Ndoto ya Diamond Yazidi Kung'aa Sasa Apata Nafasi Billboard


Moja ya ndoto nyingi za mastaa kibao wa muziki ni kupata nafasi Billboard. Diamond Platnumz amepata bahati hiyo baada ya kuandikwa kwenye makala ya mtandao wa Billboard.

Katika picha ambayo imewekwa kwenye makala hiyo, Diamond amewekwa pamoja na wasanii wengine wanne kutoka Afrika Magaribi akiwemo Wizkid, Davido na Tiwa Savage.
Kwenye makala hiyo ambayo imewaonyesha wasanii hao inazungumzia juu ya lebo kubwa za muziki duniani zinavyoangazia Afrika kumpata staa ajaye wa Pop duniani.

Hilo limekuja ikiwa ni siku chache zimepita baada ya kampuni ya Universal Music Group ambayo pia inasimaamia kazi za Diamond, kupitia tawi lake la nchini Uholanzi ilitangaza kununua hisa asilimia 70 za lebo ya AI Records ya nchini Kenya.

UMG watakuwa wanafanya kazi za kusambaza kazi za wasanii wa Al Records duniani kote ikiwemo kwenye mitandao mikubwa tofauti tofauti ya muziki.

Share:
Weka Maoni yako Hapa

0 facebook:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © MCHAMBUZI HURU | Powered by Blogger