Monday, March 5, 2018

Nabii Tito Ashindwa Kufika Mahakamani Kesi Yake Yaairishwa


Mahakama ya Wilaya ya Dodoma kesi inayomkabili Onesmo Machibya anaefahamika kwa jina  ‘Nabii Tito ‘ya kujaribu kujiua imeahirishwa hadi March 19, 2018.

Hakimu anayesikiliza kesi hiyo, James Karayemaha aliagiza mtuhumiwa huyo kuchukuliwa vipimo vya akili yake ili kujua kama ana matatizo ya akili katika taasisi ya magonjwa ya akili ya Isanga mjini Dodoma.

Leo ‘Nabii Tito’ hakuweza kufika mahakamani ambapo kesi yake iliahirishwa na Hakimu Mwajuma Lukindo.

‘Nabii Tito’ anakabiliwa na mashtaka ya kujaribu kujiua kwa kujikata na wembe na anadaiwa kufanya hivyo Januari 25, 2018 akiwa mahabusu.
Share:
Weka Maoni yako Hapa

0 facebook:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © MCHAMBUZI HURU | Powered by Blogger