Saturday, March 17, 2018

Mwanasheria Mkuu wa Serikali Nchini Marekani Amfuta Kazi Kigogo wa FBI Siku Chache Kabla ya Kustaafu


Kutoka nchini Marekani Mwanasheria Mkuu wa Serikali Jeff Sessions amemfuta kazi aliyewahi kuwa Kaimu Mkurugenzi Mstaafu wa FBI Andrew McCabe ikiwa ni siku chache tu kabla ya kustaafu rasmi na kupata haki zake zote za mafao.

Taarifa ya Sessions imeeleza kuwa McCabe amefukuzwa kazi kutokana na kuvujisha taarifa za uongo na kuwapotosha wapelelezi. Kigogo huyo wa FBI amekataa kuhusika na tuhuma hizo.

Ameeleza kuwa amezushiwa tuhuma hizo kwasababu alihusika katika kufuatilia suala la nchi ya Urusi kuingilia Uchaguzi Mkuu wa nchi hiyo mwaka 2016.

Rais Donald Trump amewahi kumtuhumu McCabe kuwa na upendeleo wa kisiasa kwa kuwa mfuasi wa Chama cha Democrats.
Share:
Weka Maoni yako Hapa

0 facebook:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © MCHAMBUZI HURU | Powered by Blogger