Friday, March 16, 2018

Muna Love Akomalia Kufuta Tatoo Zake


Msanii wa bongo movie na mjasiliamali Rose Alphonce maarufu mjini kwa jina la Munalove amefunguka na kudai kuwa atatumia zaidi ya milioni tano kufuta tatoo alizonazo mwilini m,wake.

Hatua hiyo ya kuzifuta inakuja baada ya siku za karibuni kuamua kuokoka kutokana na kupitia majaribu ya mtoto wake kuumwa.
 Munalove amesema tangu aamue kuokoka ameamua kuachana na mambo mengi ya kidunia huku tatuu ni jambo ambalo linamnyima raha na kuamua kutata kuzifuta tatoo hizo.

Amesema mpaka sasa anamichoro mitano katika mweili wake ambayo ikiwemo na Tatoo ya Shingoniambayo ni kubwa kuliko yote huku akidai kuwa ameshaulizia gharama ya kufuta na kuambiwa kuwa ni milioni tano.

''Tayari nimeshaulizia kwa wataalamu kutoka Thailand ambao watanifuta bila kupata madhara yoyote na kuniambia ni milioni tano huku hizi zingine ambazo ni ndogondogo zitakuwa chini ya milion 2.1'' Munalove

Share:
Weka Maoni yako Hapa

0 facebook:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © MCHAMBUZI HURU | Powered by Blogger