Saturday, March 3, 2018

Mtoto wa Rais Weah Ajumuishwa Kwenye Kikosi Kitakachoivaa Real Madrid


KINDA Timothy Weah, mtoto gwiji wa Paris Saint-Germain na mshindi wa zamani wa Ballon d'Or, George, amejumuishwa kwenye kikosi cha wachezaji 18 na kocha Unai Emery kuelekea mechi ijayo ya Ligue 1 dhidi ya Troyes.

Vinara hao wa Ligue 1 wanakabiliwa na mapungufu katika safu yao ya ushambuliaji kufuatia kuumia kwa Neymar, huku pia Kylian Mbappe na Edinson Cavani wote wakiondolewa kwenye kikosi cha kucheza dhidi ya Troyes.

Kocha Emery anahofia nyota wake hao wanaweza kuumia kuelekea mechi muhimu ya marudiano ya Ligi ya mabingwa Ulaya dhidi ya Real Madrid.

Kinda huyo wa umri wa miaka 18 anafuata nyayo za baba yake ambaye kwa sasa ni Rais wa Liberia ambaye enzi zake alichezea PSG kwa miaka mitatu na kushinda tuzo ya Mwanasoka Bora wa Dunia mwaka 1995 kabla ya kuhamia AC Milan.

Share:
Weka Maoni yako Hapa

0 facebook:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © MCHAMBUZI HURU | Powered by Blogger