Sunday, March 11, 2018

Mtoto wa Miaka Mitano Ampeleka Baba Yake Polisi Kisa Shamba


MTOTO mmoja mwenye umri wa miaka mitano amemfikisha katika Kituo cha Polisi Ngara, mkoani Kagera baba yake mzazi baada ya kubaini kuwa baba yake anataka kuuza kinyemela shamba ambalo ni urithi wa watoto wake.

Akizungumza baada ya kufika kituoni hapo, mtoto huyo mwenye ujasiri mkubwa alikwenda kushitaki polisi kwa msaada wa dereva wa gari  aitwae Thabiti aliyempa msaada wa lifti ya gari na kuhoji iwapoi baba yake atauza shamba, wao kama familia wataishi wapi?

Kwa upande wa mtuhumiwa ambaye ni Baba, kukamatwa na polisi na kuhojiwa amekana kuhusu kutaka kuuza shamba hilo lakini mtoto amedai ni kweli baba yake alitaka kuuza shamba.

Alipoulizwa kama anafurahia baba yake kufungwa jela kwa kosa hilo alisema hafurahii baba yake kufungwa ikizingatiwa ana mzazi mmoja tu lakini alikuwa akipigania haki yake ya shamba kutokuuzwa kwani atakosa pa kwenda kuishi.

Kwa hakika mtoto huyu ni mfano wa kuigwa katika kupigania haki na usawa katika jamii.
Share:
Weka Maoni yako Hapa

0 facebook:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © MCHAMBUZI HURU | Powered by Blogger