Friday, March 9, 2018

‘Mjomba Husein’ Mwanamke wa Kwanza Kuchimba Tanzanite Akijifanya Mwanaume


Jana March 8, 2018 ilikuwa ni Siku ya Wanawake Duniani AyoTV imempata Pili Husein au jina maarufu “Mjomba Husein”ambae ni mwanamke wa kwanza kuchimba madini ya Tanzanite katika mgodi wa Mirerani uliopo mkoani Manyara nakujifanya mwanaume kwa zaidi ya miaka 15 ili asitolewe kwenye mgodi huo kwa kuwa walikuwa hawaruhusiwi wanawake.

AyoTV na millardayo.com imempata ‘Mjomba Husein’ amesema pamoja na changamoto alizokutana nazo ameweza kuwasomesha watoto wa ndugu zake zaidi ya 32 kwa gharama zake ambapo mmoja wapo ameongoza kwenye masomo nakupata daraja la kwanza mwaka 2016 nchini Tanzania

Pamoja na hayo amempongeza Makamu wa Rais Samia Suluh Hassan kwa kumpa tuzo yakuwa mchimbaji namba moja mwanamke.

Share:
Weka Maoni yako Hapa

0 facebook:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © MCHAMBUZI HURU | Powered by Blogger