Sunday, March 11, 2018

Mechi ya Man U, Liverpool: Profesa Jay Apinga Kauli ya Steven Gerrard


Msanii mkongwe nchini ambaye hivi sasa ni Mbunge wa Jimbo la Mikumi kupitia CHADEMA Joseph Haule maarufu kama Profesa Jay amepingana na kauli ya nahodha wa zamani wa timu anayoishabikia ya Liverpool, Steven Gerrard.


Akiongea leo na East Africa Television Profesa Jay amesema kauli ya Gerrard aliyoitoa wiki hii kuwa nyota wa Liverpool Mohamed Salah ndiye mchezaji bora zaidi kutoka Africa kuwahi kucheza EPL hawezi kukubaliana nayo.

''Siwezi kuikubali moja kwa moja au kuipinga, lakini msimu huu Mo Salah amekuwa na msimu mzuri na msimu bora na tunatakiwa kujivunia kama mashabiki wa Liverpool, kikubwa nachoweza kusema Salah anaweza kuwa ni mchezaji aliyefanya vizuri zaidi katika msimu mmoja'', amesema.

Kwa upande mwingine Profesa Jay amesema kocha wa Liverpool Jurgen Klopp ameitengeneza timu hiyo kuwa moja na kufanya vizuri hivyo anahitaji muda zaidi ndani ya timu hiyo ili aweze kuipatia mataji mengi.
Share:
Weka Maoni yako Hapa

0 facebook:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © MCHAMBUZI HURU | Powered by Blogger