Monday, March 5, 2018

Mashekhe Watano Waliotoweka Zanzibar Wasimulia Baadaya Kuachiwa Huru


MASHEHE watano waliotoweka katika mazingira ya kutatanisha kuanzia Febuari 9 mwaka huu huko Zanzibar wameachiwa na kurejea katika familia zao usiku wa kuamkia jana Machi 4, 2018.

Mmoja wa Mashehe hao, Amir Khamis akifanya mahojiano na Azam TV, alisema kuwa hajui eneo walilopelekwa, lakini waliohojiwa na baada ya kuonekana hawana hatia waliachiwa bila kudhuriwa.

“Mimi na wenzangu wanne tulipelekwa kusikojulikana, baada ya kuhojiwa wametuachia tukiwa salama. Wale waliotukamata hawakuwa na nia mbaya, walikuwa wakitekeleza kazi yao ya usalama, ndiyo maana baada ya kugundua kwamba sihusiki na yale waliyokuwa wakinihoji waliniachia huru na nimerudi nyumbani, niko na familia yangu,” alisema Khamis.

Mmoja wa wanafamilia wa Shehe Khamis alisema kuwa alikuwa na hofu kwamba huenda ndugu yao hayupo hai, hivyo wamefurahi na kufarijika sana kumuona tena.

“Tulikuwa na hofu kwamba yawezekana ametupwa baharini au vinginevyo, lakini tunamshukuru sana Mungu kwa kumrejesha akiwa salama,” alisema Mke wa Shehe Khamis, Mwanaunguja Hadhar.

Share:
Weka Maoni yako Hapa

0 facebook:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © MCHAMBUZI HURU | Powered by Blogger