Monday, March 5, 2018

Marekani na Ulaya Hali si Shwari


Rais wa Marekani Donald Trump ametishia kuyatoza ushuru magari kutoka Umoja wa Ulaya, iwapo umoja huo utachukua hatua za kujibu mipango yake aliyoitangaza hivi karibuni ya kutoza kodi chuma na aluminiamu zinazoingizwa Marekani.

Kupitia ukurasa wa Twitter, Trump amesema iwapo Umoja wa Ulaya utataka kuongeza kodi ambayo tayari iko juu na kuziwekea vikwazo kampuni za Marekani zinazofanya biashara katika nchi za Umoja huo basi watayatoza kodi magari kutoka Umoja wa Ulaya yanaoingizwa Marekani.Share:
Weka Maoni yako Hapa

0 facebook:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © MCHAMBUZI HURU | Powered by Blogger