Saturday, March 3, 2018

Manara Atoa Maoni Yake Kuhusu Matokeo ya Jana


Afisa Habari wa Simba, Haji Manara, amesema timu yao imesikitishwa na matokeo ya mchezo wa jana dhidi ya Stand United, kwani hawakutegemea kama watashindwa kupata alama 3.

Manara ameeleza kuwa hakuna mwanasimba aliyefurahia matokeo na kuwataka wanachama na wapenzi wa Simba wachukulie kuwa ni matokeo ya mpira, huku akiwaambiwa hakuna timu inayoshinda kila mechi.

Aidha Manara amesema harakati zao za ubingwa wa ligi msimu huu zipo palepale, huku akieleza kuwa hakuna historia kwenye soka, kutokana na watani wao wa jadi wamekuwa wakijigamba kuwa Simba huanza vizuri na mwishoni humaliza vibaya na yanga kuutwaa ubingwa.

Hakuishia hapo, amesisitiza mipango yao ni mizuri hivyo wanaimani na matarajio yao msimu huu ni kulitwaa taji la ligi.

"Hakuna historia katika mpira, ukija na suala la kusema kwamba sisi huwa tunaanza vizuri na mwisho tunamaliza vibaya na kuepelekea kukosa taji, hakuna kitu kama hicho kwenye soka. Msimu huu tumejipanga vema na uhakika wa kutwaa ubingwa upo" amesema Manara.

Share:
Weka Maoni yako Hapa

0 facebook:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © MCHAMBUZI HURU | Powered by Blogger