Friday, March 9, 2018

Manara Ahoji Kukosekana kwa Jonas Mkude Kwenye Orodha ya Wachezaji Taifa Stars


Kocha msaidizi wa timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars Hemed Morocco kwa niaba ya kocha mkuu wa Taifa Stars Salum Mayanga ametangaza kikosi cha wachezaji 24 cha timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars kitakachocheza michezo miwili ya kirafiki iliyopo katika kalenda ya FIFA dhidi ya Algeria na DR Congo.

Baada ya kutangazwa kikosi cha wachezaji 24 na kukosekana jina la kiungo mkabaji wa Simba Jonas Mkude katika list hiyo, afisa habari wa Simba Haji Manara ameshindwa kufumbia macho na kuhoji hilo kupitia ukurasa wake wa instagram.


“Unamuachaje Jonas Mkude? mwisho wa siku sisi ni watanzania hata kama sio makocha lakini soka huchezwa hadharani, najiuliza tena na tena kwa viungo tulionao ni kweli Jonas Mkude hastahili kuitwa katika timu hii? kwa sasa hakuna ubishi Jonas Mkude ndio holding midifielder best nchini ni kumkosea heshima kuliko chumpa mpaka”
Share:
Weka Maoni yako Hapa

0 facebook:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © MCHAMBUZI HURU | Powered by Blogger