Saturday, March 10, 2018

Makonda Awaagiza Polisi Mkoa wa Iringa Wamlete Mwenyekiti wa Wanafunzi Dar Adai Amechafua Mkoa wa Iringa


Mkuu wa Mkoa, Paul Makonda amewataka Polisi wa Mkoa wa Iringa wakimalizana na Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanafunzi Tanzania (TSNP) ambaye pia ni mwanafunzi wa UDSM, Abdul Nondo aliyedaiwa kupotea kisha kupatikana mkoani Iringa, arejeshwe Dar es Salaam kwa maana ameuchafua mkoa huo.

Aidha, amewataka Waandishi wa Habari waangalie taarifa wanazopeleka kwa umma, kama hazijathibitishwa na mamlaka husika waachane nazo.

Amtaka Kamanda Mambosasa na Jeshi la Polisi kutembea kifua mbele, bila ya kuwepo kwa mtu wa kuwafedhehesha wala kuwanyong’onyesha.

Makonda amesema “Watu wanahangaika kwenye mitandao ya kijamii kutukana viongozi na kuhamasisha maandamano, nawapa pole sana. Watafanya hivyo labda mie nikiondoka lakini sio nikiwa mkuu wa mkoa,” amesema Makonda,

Amemuagiza Kamanda Mambosasa ashughulike kwa mujibu wa sheria na mtu yeyote atakayesimama na kutukana viongozi hasa kiongozi wa nchi ambaye ni Nembo ya nchi.

Share:
Weka Maoni yako Hapa

0 facebook:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © MCHAMBUZI HURU | Powered by Blogger