Thursday, March 15, 2018

Mahakama Yaishukia Upande wa Mashtaka Kesi ya Malinzi


Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imesema ni aibu kwa upande wa mashtaka kushindwa kukamilisha upelelezi wa kesi inayowakabili vigogo watatu wa TFF ambao wamekaa rumande kwa miezi tisa sasa.

Vigogo hao ni aliyekuwa Rais TFF, Jamal Malinzi, Katibu Mkuu wa TFF, Mwesigwa Selestine na Mhasibu wa TFF,  Nsiande Isawayo.

Hayo yameelezwa na Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri ambapo amesema ni aibu na ajabu kwa upande wa mashtaka kwenda mahakamani na kusema upelelezi bado haujakamilika.

“Ni miezi tisa sasa imepita bila ya upelelezi kukamilika washtakiwa wapo rumande, kinachotakiwa ni ukamilishwaji wa upelelezi wa kesi,” Amesema Hakimu Mashauri.

Pia ametupilia mbali hoja za upande wa utetezi ya kuwa Mahakama hiyo ina mamlaka ya kuwaachia washtakiwa chini ya kifungu cha 225 ,(5) cha sheria ya Mwenendo wa makosa ya jinai.

Kwa upande wa Wakili wa Malinzi na Mwesigwa, Kashindye Thabiti alilalamika mahakamani hapo kuwa wakienda magereza wanakosa uhuru wa wakuwaona wateja wao wakiwa mahabusu.

Baada ya kueleza hayo, Hakimu Mashauri ameahirishwa kesi hiyo hadi March 28, 2018 kwa ajili ya kutajwa.

Washtakiwa hao walipandishwa  kizimbani kwa mara ya kwanza June 29, 2017, wakikabiliwa na mashtaka 28 ya kughushi na kutakatisha fedha Dola za Marekani 375,418. 7.
Share:
Weka Maoni yako Hapa

0 facebook:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © MCHAMBUZI HURU | Powered by Blogger