Friday, March 16, 2018

Mafuriko Jangwani: Magari ya Mwendokasi Yashindwa Kufanyakazi Barabara Yafungwa


Abiria wa mabasi ya mwendokasi wamekosa huduma ya usafiri leo asubuhi, baada ya kampuni ya UDART kusitisha huduma hiyo kutokana na mafuriko eneo la Jangwani.

TAARIFA KWA UMMA

Kampuni inayotoa huduma katika mradi wa mabasi yaendayo haraka jijini Dar es Salaam, UDA Rapid Transit (UDART), inaujulisha umma kuwa, huduma za mabasi hayo zimesitishwa kuanzia saa 11:00 alfajiri tarehe 16/03/2018 kutokana kufungwa kwa Barabara ya Morogoro eneo la Jangwani kwa sababu ya mafuriko yaliyosababisha maji kupita juu ya daraja la Mto Msimbazi.

Huduma zitarejea mara baada ya barabara kufunguliwa. Tunaomba radhi kwa usumbufu uliojitokeza.

Share:
Weka Maoni yako Hapa

0 facebook:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © MCHAMBUZI HURU | Powered by Blogger