Saturday, March 17, 2018

Maandamano ya Aprili 26 Bado Yampasua Kichwa Makonda Ampa Salamu Meya wa Jiji Kumpelekea kwa Mbowe


Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amemtuma meya wa jiji kuzungumza na viongozi wake wa chama(Chadema) kufikiria upya kuhusu hali ya usalama katika jiji hilo ili kufanikisha ukuzaji wa sekta ya utalii katika jiji hilo.

“Mstahiki meya wa jiji, leo tunazindua utalii wa ndani na tumemuita waziri wa Tamisemi atuzindulie, kawaulize ndugu zako wale akina Mbowe (Mwenyekiti wa Chadema) na akina nani wale, waulize...wakifanya vurugu, hawana watalii watapita mji gani?”Amehoji Makonda  leo Machi 17, 2018 wakati wa mkutano wa kuzindua utalii wa ndani katika mkoa huo.

Katika hatua nyingine, Makonda ametoa maagizo manne katika kufanikisha utalii wa ndani katika jiji hilo akisema, kwanza ni lazima kuhamasisha utalii huo, kuendeleza usafi katika jiji hilo, kuboresha vituo vya mabasi yaendayo mikoani.

Katika hatua nyingine, Makonda ameahidi kuzindua viwanda 200 katika jiji hilo hapo baadaye badala ya viwanda 100 vilivyoagizwa na Serikali katika kila mkoa

“Ulitupatia maelekezo ya kila mkoa viwanda 100, mie nakuahidi , nitakualika mwenyewe kuzindua ujenzi wa viwanda 200 kwa wakati mmoja, tumeshapata wawekezaji na sasa tuko kwenye mchakato wa kukamilisha suala la ardhi,”amesema Makonda.

Awali, Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam, Spora Liana ametaja mipango kadhaa iliyoanza kutekelezwa na jiji hilo katika kukuza na kuimarisha sekta ya utalii.

Share:
Weka Maoni yako Hapa

0 facebook:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © MCHAMBUZI HURU | Powered by Blogger