Monday, March 5, 2018

Kwa Mara ya Kwanza Wanawake Washiriki Katika Mashindano ya Kukimbia Saudi Arabia


Wanawake nchini Saudi Arabia kwa mara ya kwanza katika historia wameshiriki mashindano ya kukimbia.

Kwa mujibu wa habari,mashindano hayo ya kilomita 3 yamefanyika  mashariki mwa Al Ahsa.

"Al-Ahsa Runs" lilikuwa jina la marathon, ambalo lilihusisha wanawake 1,500 katika makundi mbalimbali kama vile kitaaluma, amateur, wazee na vijana.

Mkurugenzi Mkuu wa Michezo wa Saudi Arabia ,Hospitali ya Al-Moosa na hospitali ya manispaa ya al-Ahsa wamedhamini mashindano hayo.

Mizna al-Nassar wa Saudi Arabia alishinda medali ya kwanza katika marathon, akiwaacha nyuma wapinzani wake kutoka katika mataifa tofauti.

Share:
Weka Maoni yako Hapa

0 facebook:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © MCHAMBUZI HURU | Powered by Blogger