Monday, March 12, 2018

Kwa Kipigo Hiki! Wenger Atabaki?


Arsenal imefanikiwa kuiadhibu Watford magoli matatu. Kipigo hiki kinaipa Arsenal nafasi nzuri ya kurudi michuano ya Yuropa hapo mwakani. Shukrani za Pekee zimwendee Petr Cech aliyefikisha rekodi ya kutokufungwa katika michezo 200 ya ligi kuu baada ya kuokoa mkwaju wa Penalti Troy Deeney.

Piere Aubameyang alimpiga chenga golikipa na kuiandikia Arsenal bao la pili. Henrekh Mkhtaryan alifunga goli la tatu na kuipa Arsenal uhakika wa ushindi.
Hii ni Penati ya kwanza kwa Petr Cech kuokoa tokea mwaka 2011. Mara ya mwisho alidaka Penati dhidi ya Fulham. ni penati yake kwa 16 akiwa na Arsenal na ni penati ya kwanza akiwa kama mchezaji wa Arsenal.

Ozil amekuwa mchezaji wa kwanza kufikisha asisti 50 kwa haraka zaidi akiwa amecheza michezo 141 na kuvunja rekodi ya Eric Cantona aliyecheza michezo 143. Huu ni ushindi wa 700 kwa Arsene Wenger katika michezo 1222. Kufikia hapo Arsenal wamebakiza alama 10 ili kwenda Top Four licha ya kucheza mechi nyingi zaidi.

Kituko kikubwa ni mashabiki wa Arsenal kususia mchezo kwa kile wanachodai ni kutofurahishwa na mwenendo wa matokeo mabovu ya klabu hiyo. Mashabiki walio wengi wameonekana kuchoshwa kabisa na Arsene Wenger wakimtaka aachie hatamu kwa ajili ya mwalimu mwingine.

Tatizo kubwa mashabiki wa Arsenal wamekuwa na kusumba ya kukosa msimamo hasa pale timu yao inapopata matokeo chanya husahau vilio vyao. Je awamu hii watakubaliana na Wenger? Hasa baada ya kutoa kichapo kwa Ac milan ugani sansiro?

Share:
Weka Maoni yako Hapa

0 facebook:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © MCHAMBUZI HURU | Powered by Blogger