Sunday, March 11, 2018

Kubenea Afunguka Mazito Baada ya Kufukuzwa Kwenye Ofisi Yake


Mbunge wa Ubungo Saed kubenea amesema Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Ali Hapi kumufukuza kwenye Ofisi yake ya ubunge iliyokuwa Katika manispaa ya Kinondoni ni kujitafutia ujiko kwa wakubwa wake wa kazi ili apandishwe cheo.

Kubenea ameyasema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari Ofisini kwake Kinondoni na kubainisha kuwa kwa sasa umezuka mtindo kwa watumishi wa umma kugombana na wabunge wa upinzani ili wapandishwe vyeo.

Ameongeza kuwa ni kweli amefukuzwa katika ofisi hizo na kwamba tayari  amekwishapata ofisi nyingine katika eneo la ubungo maeneo ya majengo ya urafiki.

Hivi karibuni Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Ali Happi aliwafukuza katika ofisi zao wabunge wote walikuwa wakitumia jengo la mkuu wa wilaya kwa madai kuwa anataka kuzitumia ofisi hizo kwa matumizi ya serikali.
Share:
Weka Maoni yako Hapa

0 facebook:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © MCHAMBUZI HURU | Powered by Blogger