Monday, March 12, 2018

Kiongozi Mwingine Bavicha Ajiuzulu


Dar es Salaam. Naibu Katibu Mkuu wa Baraza la Vijana la Chadema (Bavicha), Gertrude Ndibalema amejiuzulu wadhifa huo kuanzia jana Machi 11,2018.
Gertrude aliyeshika wadhifa huo tangu mwaka 2014 ametangaza kujiuzulu kupitia taarifa kwa umma akidai anabaki kuwa mwanachama ili kutimiza majukumu yake binafsi.
Soma: ‘Madiwani waliojiuzulu Chadema walitokana na mafuriko ya 2015’
Akizungumza na Mwananchi leo Machi 12,2018 Gertrude amesema, “Ni kweli nimeamua kuachia nafasi yangu ili kutimiza malengo ya shughuli zangu binafsi.”
“Kwa kuwa nakipenda chama changu na kwa taaluma yangu (mawasiliano kwa umma) ili kuepuka mgongano, nimeamua kukaa pembeni ili kutimiza azma yangu na nitabaki kuwa mwanachama,” amesema.
Gertrude ni kiongozi wa pili wa ngazi ya juu Bavicha kujizulu akitanguliwa na aliyekuwa mwenyekiti wa baraza hilo, Patrobas Katambi aliyejiunga na CCM.

Share:
Weka Maoni yako Hapa

0 facebook:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © MCHAMBUZI HURU | Powered by Blogger