Monday, March 5, 2018

KCMC Yafunguka Kuhusu Maendeleo ya Hali ya Mbowe


Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe aliyelazwa katika Hospitali ya Rufaa ya KCMC anasumbuliwa na maumivu makali ya kichwa, ameekeza Afisa Habari wa KCMC.

Ofisa habari wa KCMC, Gabriel Chisseo amesema hayo leo Machi 5,2018 alipozungumza na waandishi wa habari.

Chisseo amesema walimpokea Mbowe jana jioni Machi 4, 2018 akiwa na maumivu makali ya kichwa.

Amesema hali ya Mbowe inaendelea vizuri na amepumzishwa hospitalini hapo.

“Jana jioni tulimpokea Mbowe, taarifa zinaonyesha alikuwa na maumivu ya kichwa. Taarifa za kitabibu zinaonyesha ni uchovu,” amesema Chisseo.

Amesema madaktari wanaendelea kumhudumia kwa ukaribu na baadaye atafanyiwa vipimo vingine.
Share:
Weka Maoni yako Hapa

0 facebook:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © MCHAMBUZI HURU | Powered by Blogger