Saturday, March 17, 2018

Irine Uwoya Afunguka Sababu za Mama yake Kutojihusisha na Ndoa YakeIrene Uwoya Atoa Sababu ya Mama Yake Kutoshiriki Kwenye Ndoa Yake
Muigizaji, Irene Uwoya amefunguka sababu mama yake kutoshiriki kwenye ndoa yake na Dogo Janja.

Irene Uwoya ameiambia Leo Tena ya Clouds Fm, kuwa mama yake amekuwa ni mtu wa kusafiri mara kwa mara hiyo ndiyo sababu iliyopelekea kutompeleka Dogo Janja nyumbani.

“Hakuwepo kwahiyo hakuweza kushiriki kwasababu mama angu ni mtu wa kusafiri sana kwahiyo hakuwepo Tanzania lakini ndoa ameibariki. Mama anaenda anarudi kazi zinakuwa nyingi, kwahiyo hatujapata nafasi ya kusema sasa katulia twende bado, lakini tunaendaga mimi na yeye nyumbani mama anakuwa hayupo sometime baba anakuwepo ,” alisema Irene.

Hata alivyoulizwa kutokuwepo kwa ndugu zake kwenye ndoa yake Irene ameeleza kuwa ndugu zake walikuwepo baadhi japo hawakuwa wengi.

Share:
Weka Maoni yako Hapa

0 facebook:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © MCHAMBUZI HURU | Powered by Blogger