Monday, March 5, 2018

Ikulu Yakanusha Kumtengua Dkt. Kigwangalla


Serikali ya awamu ya tano ya Rais Dkt. John Magufuli imekanusha taarifa ya kutenguliwa kwa uteuzi wa Waziri wa Maliasili na utalii Dkt. Hamis Kigwangalla na kuitaka jamii kuzipuuza endapo watakutana nazo mitandaoni.

Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais- Ikulu, Gerson Msigwa asubuhi ya leo katika ukurasa wake maalumu wa kijamii na kusema taarifa hizo ni uzushi mtupu hazina ukweli wowote.

Jana (Machi 4, 2018) ilisambazwa barua iliyokuwa inaonesha kutoka Ikulu ambayo imeandika taarifa za kutenguliwa uteuzi wa Waziri huyo huko sababu kuu zilizokuwa zimeainishwa ni kutokana na kauli iliyotolewa na Dkt. Kigwangalla huko Mkoani Kagera ikihamasisha watumishi wa wizara hiyo iliyo chini yake kujichukulia sheria mkononi dhidi ya raia wa mataifa jirani.

Share:
Weka Maoni yako Hapa

0 facebook:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © MCHAMBUZI HURU | Powered by Blogger