Thursday, March 1, 2018

Hii ndio sababu ya Davido kumtaja Ronaldo mara kwa mara kwenye nyimbo zake


Kama wewe ni mfuatiliaji wa nyimbo za Davido bila shaka utakuwa umeshawahi kusikia baadhi ya nyimbo zake kama FALL na AYE akimtaja mchezaji wa Klabu ya Real Madrid, Cristiano Ronaldo, sasa ukweli ni kwamba Davido ana ndoto siku moja kuja kufanya naye kazi.

Akihojiwa kwenye kipindi kipya cha Goal Playlist kinachorushwa kwenye YouTube Channel ya  mtandao wa habari za michezo wa GOAL.COM aliulizwa unamjuaje Ronaldo?, Davido alisema ni rafiki yake lakini hajawahi kukutana naye kutokana na ubize wa wote wawili ila ana mipango ya kufanya naye kazi.

“Ndiyo ni rafiki yangu lakini sijawahi kukutana naye, unajua yeye yupo bize na mimi nipo bize, Nadhani nitafanya naye video, ila sitaki kusema itakuwa ni video ya muziki, najitahidi kuwaza kufanya kitu ambacho kitawakutanisha watu wetu duniani kote,“amesema Davido.

Je, itakuwa ni video ya aina gani ambayo Davido atafanya na Ronaldo? tusubiri kuona kwani hata Tanzania, Diamond Platnumz naye ni moja ya wasanii waliowahi kumtaja Ronaldo kwenye nyimbo zake lakini kwa mapenzi yake binafsi.
Share:
Weka Maoni yako Hapa

0 facebook:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © MCHAMBUZI HURU | Powered by Blogger