Friday, March 16, 2018

Haya Ndiyo Mauaji Makubwa ya Halaiki Yaliyowahi Kutokea Duniani


Ukisikia mauaji ya Halaiki (genocide) akili inakimbilia Rwanda , Soweto na Holocaust (waisrael walivyouliwa na WANAZI). Leo tunakupa Mauaji yaliyosahaulika lakini nayo ni makubwa mno.

1. WAJERUMANI WALIVYOSAFISHA KABILA LA WAHERERO.
Baada ya kusikia fununu ya madini Namibia, Wajerumani walikuja na kutawala pwani ya nchi hiyo na kukaa katikati ya kabila la waherero. Kosa kubwa wenyeji walipojifanya wabishi. Walizungukwa pande zote, Upande uliobaki ulikuwa ni jangwa ambalo visima vyote vya maji mjerumani alivitia sumu. Ukimbie unywe maji ya sumu au ufe na kiu jangwani au ukutane na risasi. Asilimia 80 ya wenyeji wote waliuwawa kikatili sana bila huruma.

2. WASOVIETI/USSR WALIPOHAMISHA JAMII NZIMA YA WACHECHNYA.
Kulizuka fununu kuwa Wachechya na Wainguish walikuwa wanawasaliti warusi wenzao vita ya pili ya dunia. Kuwapa adhabu serikali iliamuwa kubeba wote kwenye magari na kuwafukizilia maporini bila kumsamehe hata mmoja. Kila aliyebisha alikutana na Risasi . Wachechnya waliuwawa karibu 50% kutokana na sakata hili lililoitwa “Operation Lentil.”.

3. (HAITI) MAUWAJI YA PARSLEY/EL CORTE AU (KUKATWA).
Ukabila usikie tu redioni. Hii ilikuwa ni vita ya Kikabila, Wadominika walipanga kuwauwa Wahaiti karibu wote nchini mwao chini ya dikteta Rafael Leonidas Trujillo. Njia pekee ya kumtofautisha Mdominika na Muhaiti kwa walioleta utata kuwatambua ilikuwa matamshi ya hili neno "PARSLEY". Wahaiti walikuwa hawawezi kulitamka vizuri kutokana na Lugha yao. Wote walioshindwa waliuwawa kinyama. Kuepusha risasi zisiishe mapema, Hapa ilikuwa ni Mapanga na marungu asubuhi na mchana.

4. (TAIPEI REBELION) CHINA WATU ZAIDI YA 20 MILLION WALIPOTEZA MAISHA.
Hapa ilikuwa ni vita kati ya jamaa aliwaaminisha watu kuwa yeye ni Mdogo wake YESU. Akitawala karibu 1/3 ya nchi yote Hong Xiuquan. Akiongoza jeshi dhaifu kabisa kwa nia ya kuondoa kamali, uonevu, ndoa za wake wengi nk, China ilijikuta chini aya vita vya miaka 10 na kuacha raia zaidi ya 200 million wakifa na mamia kupotea.

5. UTURUKI DHIDI YA WANAVIJIJI WAASI.
Wanakijiji wa eneo la Dersim , walipoleta ubishi kuwa chini ya serikali ya Uturuki badala yake wakang'ang'ania sheria na taratibu zao, Jeshi lilitumwa, Makabila matatu yaliyojisalimisha yaliuliwa wote, Wakina mama na watoto waliokimbilia kwenye Mapango, Yalifunikwa na mawe, moto ukawashwa na wakafa kwa moshi. Inakadiliwa kwa siku moja watu karibu 2 MILLION waliuliwa na wengine kutekwa.

6. DICTETA WAKIRUSI STALIN ALIPOUA MAMILIONI UKRAIN KWA NJAA.
Waukraini walipata upenyo baada ya kuanguka utawala wa Czar Urusi wakataka kujitawala. Jenelali Stalin alipochukua Madaraka akaliona hilo. Pia Vradmil Lenin alikuwa kaishaweka mikakati ya kurudisha maeneo yote. Wao wakambishia na kuendelea na Harakati. Kwanza alikamata wasomi waliokuwa wanahojihoji 5000 na kuwaua wote, Akachukua mashamba ya raia yote. Akawapa adhabu ya njaa hadi nchi nzima isalimu amri kwake. Inasadikiwa kwa sababu ya njaa kila siku watu 2500 walikuwa wanakufa, na walifika watu karibu million 5.

7. MAUAJI YALIYOFANYA NA WAZUNGU DHIDI YA WAMAREKANI ASILIA (WAHINDI WEKUNDU).
Mamilioni ya hawa jamaa waliuliwa bila huruma. Ila hapa tutazaungumzia kabila dogo tu la MOQUI katika mji ulioitwa AWATOVI huko ALIZONA. Wahispania Makasisi walifika wakawalazimisha kuwa wakristo wakagoma. Ikabidi liitwe jeshi, maana wakazi waliwachukia wahispania na wachache waliobadili dini. Wanaume wakiwa kwenye sherehe Walivamiwa na kuuliwa. Wanaume wote. Wanawake na watoto wakachukuliwa mateka. Wakiwa njiani wakabishana wawapeleke wapi, wakaamua kuwaua woote ili kujipunguzia mizigo.

8: JEAN JACQUES DESSALINES ALIPOIGEUZA HAITI KUWA TAIFA LA WATU WEUSI ASILIMIA MIA.
Kile alichoshindwa kinjekitile wa Maji maji Haiti iliwezekana. Mzungu alikimbizwa na watumwa nchi ikapatia uhuru chini ya mkono wa watu weusi. Baada ya kiongozi wa mapinduzi kuuawa aliyemfuatia alipinga idea zake za kuwavumilia wazungu na machotara. Amri ilitolewa Kuua wazungu wote nchi nzima. Hakuishia hapo tu alipita kila mji kuhakikisha agizo linafuatwa. Katika mji mkuu tu wazungu zaidi ya 800 waliuawa kama wanyama na wengine kukimbia. Ilikuwa revenge ya aina yake. Hadi kesho haiti ni nchi ya watu weusi tu asilimia karibu mia kwa baara la Barani Amerika.

9: VITA VYA BIAFRA - NIGERIA.
Tofauti na tanzania tuna makabila mengi yanayopendana, na Nyerere alisaidia kikubwa, Hii haikuwa hivyo Nigeria. Wanamakabila zaidi ya 300 na yalikuwa karibu karibu kilichosababisha ugomvi mara kwa mara.Tatizo lilianza pale Kabila/kundi kubwa la IGBO walipojikatia nchi na kutengeneza nchi yao ya BIAFRA eneo tajiri kwa mafuta. Serikali haraka ikataka kuwarudisha. Kwa mbinu katili kabisa hata kuzuia chakula na maji yasielekee BIAFRA. Inasemekana kila siku walikuwa wanakufa watu zaidi ya 5000 wengi wao IGBO. Watu zaidi ya Milioni 3 walikufa hadi vita kuisha.

Share:
Weka Maoni yako Hapa

0 facebook:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © MCHAMBUZI HURU | Powered by Blogger