Thursday, March 15, 2018

HAWA Watu Ndani ya Serikali Hawamuogopi Mungu - Prof Tibaijuka


Mbunge wa Muleba Kusini(CCM), Anna Tibaijuka amefunguka na kusema kuwa wapo watu ndani ya Serikali ya awamu ya tano hawamuogopi Mungu ndiyo maana wanakuwa wanawaonea wananchi na kuichafua serikali pamoja na Rais Magufuli.


Tibaijuka amesema hayo wakati akiongea na wananchi katika mkutano wa hadhara baadaa ya kuona watu wakilipishwa kodi na kupewa risiti za mwaka 2015 fedha ambazo zinaonekana hazifiki serikalini.

"Serikali ya Rais Magufuli haiwezi kukubali haya mambo wanataka tu kuchafua jina la Rais amini usiamini serikali zinahujuma ndani yake sasa watu wanatokaje Mwanza na kumlazimisha huyu mvuvi mkubwa ambaye ana mitumbwi 28, anakuja mtu mla rushwa serikali ya Magufuli haiwezi kumtoa mtu kule aje kula rushwa huku, Rais Magufuli huyu anayelia usiku na mchana mambo yakae vizuri ila leo nitamtumia risiti zile za watu wake wamekusanya kodi hapa kwa risiti za mwaka 2015" alisema Tibaijuka

Aidha Tibaijuka amesema kuwa yeye anaamini kuwa Rais Magufuli hawezi kutuma watu kwenda kuchoma nyavu za wavuvi

"Yaani wamemkuta mvuvi yupo stoo anaendelea na mafundi wake kurekebisha hawa watu ambao hata hawamuogopi Mwenyezi Mungu wanaingia mle stoo na kuchoma zile nyavu, sasa watu wanasema siku za mwizi arobaini" alisema Tibaijuka
Share:
Weka Maoni yako Hapa

0 facebook:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © MCHAMBUZI HURU | Powered by Blogger